Dodoma FM

Serikali yachukua hatua kudhibiti Korongo la Shaban Robert Mpwapwa

9 July 2026, 16:52

Baadhi ya wakazi wamesema wamefurahishwa na hatua hiyo.Picha na Mtandao.

Ufanisi wa udhibiti wa korongo hilo unategemea pia utunzaji wa mazingira katika maeneo ya milima.

Na Stephen Noel. 

Wananchi wa Mitaa ya Majengo, Hazina na Vighawe Wilayani Mpwapwa, Mkoa wa Dodoma wameipongeza Serikali kwa kuanza hatua za kudhibiti korongo la Shabani Robert lililosababisha uharibifu wa baadhi ya nyumba za wakazi hao.

Wakizungumza na DODOMA FM, baadhi ya wakazi wamesema wamefurahishwa na hatua hiyo lakini wameiomba Serikali kutafuta suluhisho la kudumu kwa kushughulikia chanzo cha tatizo hilo.

Kwa upande wake, Msimamizi wa mradi kutoka Kampuni ya Mtwivila Construction Company Limited, Bw. Elivan Mahendahenda, amesema ufanisi wa udhibiti wa korongo hilo unategemea pia utunzaji wa mazingira katika maeneo ya milima.

Wananchi wameomba wadau wa mazingira na Serikali waendelee na kampeni za upandaji miti na ujenzi wa matuta ili kupunguza athari za mmomonyoko wa udongo katika wilaya hiyo.

Sauti ya kina Noel.