Wanafunzi watakiwa kuto fumbia macho vitendo vya ukatili
18 August 2026, 16:53

Mpwapwa sekondari ni miongoni mwa shule inayojunuisha Wanafunzi kutoka mikoa mbalimbali na shule ya bweni ambayo pia ni shule ya jumuishi.
Na Stephen Noel.
Jeshi la Polisi wilaya ya Mpwapwa kitengo cha dawati la jinsia limewataka Wanafunzi wa shule za sekondari kuto nyamazia vitendo vya ukatili vinavyotokea Katika Maeneo Yao Bali wayatolee taarifa Ili yaweza kuyathibitiwa.
Wakitoa Elimu ya ukatili Katika shule ya sekondari Mpwapwa Askari hao wamesema sehemu nyingi za mikosanyiko ndio sehemu ambazo zinaweza weza kuwa vyanzo vya ukatili hivyo wasisite kutoa taarifa ya vitendo hivyo.
Baadhi ya Wanafunzi wamesema aina ya ukatili unaweza kutoka Katika Maeneo ya shule ni ukatili wa kingono,ukatili wa kimwili,ukatili wa kisaikolojia na ukatili wa kiuchumi.