Dodoma FM

Wajawazito wahimizwa kuzingatia elimu ya afya ya uzazi

18 September 2026, 17:02

Pichani mwana mama mjamzito akipatiwa hudumua kwaajili ya maendeleo ya mama na mtoto. Picha na UN News.

Familia imetakiwa kupata elimu na kupanga uzazi kwa kutumia njia salama na zinazotambulika kitabibu, huku wanawake wakihimizwa kufika katika vituo vya afya kwa ajili ya kupata ushauri na huduma stahiki ili kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza wakati wa ujauzito.

Na Daniel Njau.

Elimu ya afya ya uzazi imetajwa kuwa muhimu katika maisha ya mwanamke na mwenza wake, hususan katika kipindi cha kujiandaa kupata ujauzito na wakati wa ujauzito, ambapo huduma mbalimbali hutolewa katika vituo vya afya.

Baadhi ya wanawake bado hukabiliwa na changamoto zinazowafanya kusita kufika hospitalini kupata huduma za afya ya uzazi. Changamoto hizo ni pamoja na hofu zinazohusiana na umri pamoja na namna wanavyopokelewa na baadhi ya wahudumu wa afya, hali inayoweza kuwafanya kutofuata ushauri wa wataalamu.

Mtaalamu wa afya ya uzazi kwa wanawake Bwana John France amesema huduma za afya ya uzazi humsaidia mama mjamzito katika kipindi cha ujauzito kwa lengo la kuhakikisha usalama wake na wa mtoto aliye tumboni. Ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili baadhi ya wanawake ni ukosefu wa elimu sahihi kuhusu uzazi wa mpango.

Simulizi na Daniel Njau.