Dodoma FM

Wananchi watakiwa kutumia nishati safi kutunza mazingira

3 September 2026, 16:46

Matumizi ya nishati safi kama gasi na umeme yanalenga utunzaji wa mzingirana afya ya viumbe hai katiaka jamii. Picha na mtandao.

Baadhi ya wananchi wanaotumia nishati mbadala wamesema imekuwa na manufaa katika maisha yao ya kila siku, hasa katika kupikia, kutokana na kuwa rahisi kutumia na kusaidia kupunguza utegemezi wa vyanzo vya nishati vinavyoweza kuathiri mazingira.

Na Daniel Njau.

Uelewa wa wananchi kuhusu matumizi ya nishati mbadala umetajwa kuwa muhimu katika kulinda mazingira na kufikia maendeleo endelevu, huku baadhi yao wakieleza kuwa gharama na ukosefu wa elimu ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha matumizi yake.

Baadhi ya wananchi wamesema licha ya kuwepo kwa elimu kuhusu nishati mbadala, baadhi ya watu bado hawajachukua hatua kuitumia, huku gharama za teknolojia hiyo zikitajwa kuwa sababu nyingine ya wananchi wengi kuendelea kutumia vyanzo vya kawaida vya nishati.

Mtaalamu wa miundo ya vifaa vya nishati, ikiwemo biogas, Godwin Migwa, amesema nishati jadidifu ni vyanzo vya nishati vinavyoweza kutumika bila kuisha kwa urahisi na havichafui mazingira, akitaja nishati ya jua, upepo, taka, biomasi na maporomoko ya maji.

Amesema pamoja na hayo bado kuna upungufu wa wataalamu pamoja na vyuo vinavyotoa mafunzo ya teknolojia hiyo.

Sauti na Daniel Njau.