Matumizi ya akili unde yanavyoweza leta ufanisi katika shughuli mbalimbali
10 August 2026, 16:11

Wakati matumizi ya akili unde yakizidi kuenea duniani, wataalamu wanaendelea kusisitiza umuhimu wa matumizi yenye uwajibikaji ili teknolojia hiyo iwe chachu ya maendeleo, ubunifu na fursa mpya za ajira badala ya kuwa chanzo cha changamoto kwa jamii.
Na Kang’wa Mangala.
Imeelezwa kuwa matumizi ya akili unde imeendelea kuleta mijadala kuhusu mchango wake katika maisha na ajira kwa vijana.
Wakizungumza baadhi ya vijana Jijini Dodoma wamesema kuwa, licha ya kuwa akili unde inaleta ufanisi katika utendaji kazi lakini ikitumika vibaya inaweza kuleta matokeo hasi katika ubunifu wa fikra.
Daktari Deo Shao mhadhiri kutokea Chuo Kikuu Cha Dodoma ameeleza kuwa akili unde ikitumika vyema inaleta ufanisi katika shughuli za binadamu. Na kuiasa jamii juu ya matumizi ya programu hio.