Dodoma FM

Wakulima wa zabibu Dodoma walia na soko

24 August 2026, 17:18

Zabibu zikiwa shambani mkoani dodoma, huku wakulima wakitaka bei na masoko ya uhakika kwa zao hilo. Picha na Mtandao.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo imehimizwa kuendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara, kuboresha miundombinu ya masoko na kutafuta fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi, ili zao la zabibu liendelee kuwa nguzo muhimu ya kuinua uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla.

Na Derick Mazemba

Zao la zabibu, linalotambulika kuwa miongoni mwa mazao ya kimkakati mkoani Dodoma, limeendelea kukabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa bei na soko la uhakika, hali inayowakatisha tamaa wakulima na kuathiri juhudi zao za kujikwamua kiuchumi.

Baadhi ya wananchi na wakulima wa zabibu wameeleza kusikitishwa na hali hiyo, wakisema gharama za uzalishaji wa zao hilo zimekuwa kubwa ikilinganishwa na bei wanayopata sokoni, jambo linalopunguza faida na tija ya kilimo hicho.

Akizungumzia changamoto hiyo, mjumbe wa Chama cha Wakulima cha UWAZAMAM amesema kuna umuhimu kwa Serikali na wadau wa kilimo kuingilia kati kwa kuweka mikakati madhubuti itakayowawezesha wakulima kupata bei elekezi inayolingana na thamani halisi ya zao la zabibu.

Kwa upande wake, Afisa Masoko amewashauri wakulima kuzingatia uongezaji thamani wa zabibu pamoja na kujiunga katika vyama vya ushirika imara, ili kuwawezesha kuwa na sauti ya pamoja katika kutafuta masoko na kupanga bei yenye tija badala ya kuuza mazao yao mmoja mmoja.

Sauti na Derick Mazemba.