Dodoma FM

Serikali kuanza ujenzi wa chuo mahiri cha Tehama jijini Dodoma

29 January 2024, 8:59 pm

Picha ni katibu mkuu wizara ya habari mawasiliano na teknolojia ya habari Bw Khamisi Mohammed wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa halmashauri ya Jiji uliopo Mtumba jijini Dodoma. Picha na Thadei Tesha.

Mradi huo unatarajia kuhusisha ujenzi wa vyuo viwili katika eneo la Nala jijini Dodoma Na mkoa wa kigoma.

Na Thadei Tesha.
Serikali kupitia Wizara ya habari na Teknolojia ya habari inatarajia kuanza ujenzi wa chuo mahiri cha Tehama katika eneo la Nala Jijini Dodoma ikiwa ni pamoja na kutoa fursa ya ufadhili wa mafunzo ya Tehama kwa watumishi wa umma 400.

Hayo yamesemwa na katibu mkuu wa wizara ya habari mawasiliano na teknolojia ya habari Bw Khamisi Mohammed wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa halmashauri ya Jiji uliopo Mtumba jijini Dodoma

Amesema kuwa mradi huo unatarajia kuhusisha ujenzi wa vyuo viwili katika eneo la Nala jijini Dodoma Na mkoa wa kigoma ambapo ujenzi huo utasaidia kuchochea maendeleo ya viwanda ambayo ni chachu ya ukuaji wa uchumi wa kidigitali duniani

Sauti ya Bw Khamisi Mohammed.

Baadhi ya wadau katika sekta ya elimu wakiwemo wakuu wa vyuo kutoka chuo kikuu cha Dodoma na chuo kikuu cha sayansi Mbeya ni baadhi ya wadau walioshiriki katika ufunguzi huo ambapo wamesema kuwa ujenzi wa chuo hicho ni muhimu hivyo wataendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika suala La maendeleo ya Tehama Nchini.
Insert………………………..

Sauti za wakuu wa vyuo kutoka chuo kikuu cha Dodoma na chuo kikuu cha sayansi Mbeya