Dodoma FM

Wananchi na Serikali watakiwa kuzingatia na kuzilinda haki za binadamu

20 August 2021, 11:15 am

Na; Benard Filbert.

Serikali pamoja na wananchi wameombwa kuzingatia na kuzilinda haki za binadamu ili kuepusha uvunjifu wa amani katika jamii.

Hayo yameelezwa na mwanasheria Daniel Mayula kutoka taasisi ya SAUTI YANGU ambayo imekuwa ikijihusisha na utetezi wa haki za binadanmu wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu umuhimu wa kuzingatia haki za binadamu.

Bw. Daniel ameiambia taswira ya habari haki za binadamu zinatakiwa kuzingatiwa na kila mtu kuanzia Serikali pamoja na wananchi kwani katiba inatambua haki hizo na imeelezwa katika ibara ya 12 hadi 29.

Amesema changamoto iliyopo ni baadhi ya wakazi hasa maeneo ya vijijini wamekuwa wakivunjiwa haki zao za binadamu lakini wanakosa sehemu za kutolea taarifa.

Baadhi ya wakazi katika Jiji la Dodoma wakizungumza na Taswira ya habari wamesema ni vyema elimu ikatolewa vya kutosha kwa kila mmoja ili wajue na kuzitambua haki za binadamu kwa ujumla kwa wakazi wa maeneo ya mijini na vijijini.

Jamii inasisitizwa kutoa taarifa katika maeneo husika pale wanapoona uvinjifu wa haki za binadamu kutokana na haki hizo kuwepo kwa mujibu wa sheria.