Dodoma FM

Jamii yaeleza kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya vifaa vya kuzima moto

9 August 2023, 3:22 pm

Mmoja wa wataalamu wa vifaa vya kuzimia moto  kutoka jeshi la zimamoto na uokoaji akielekeza jinsi ya kutumia kifaa hicho. Picha na Thadei Tesha.

Jeshi la zimamoto na uokoaji limekuwa kikisisitiza matumizi ya vifaa hivi katika jamii ingawa baadhi ya wananchi wanasema kuwa ipo haja kwa jeshi hilo kuongeza nguvu ili elimu hiyo izidi kuwafikia wananchi wengi.

Na Thadei Tesha.

Ili kukabiliana na majanga mbalimbali ikiwemo majanga ya moto yanayotokea mara kadhaa katika jamii Imeelezwa kuwa bado elimu ya matumizi ya vifaa vya kuzimia moto si ya kutosha.

Miongoni mwa kifaa maarufu kinachotumika kuzimia moto ni pamoja na kifaa hiki ambacho ni maarufu kwa lugha ya kingereza kama fire extinguisher nawauliza baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma je ni kwa kiasi gani wanakifahamu kifaa hiki?

Sauti ya Mwananchi.
Mmoja wa wataalamu wa vifaa vya kuzimia moto  kutoka jeshi la zimamoto na uokoaji akiongea na Dodoma Tv. Picha na Thadei Tesha.

Aidha wanatoa ushauri kwa serikali pamoja na jeshi la zimamoto na uokoaji juu ya mbinu za kutumia ili elimu hii iwafikie wananchi kwa kiasi kikubwa kwani wengi wao huishia kukiona tuu katika maeneo mbalimbali.

Sautin za wananchi

Jeshi la zimamoto na uokoaji ni moja ya taasisi yenye dhamana ya kutoa elimu kwa jamii juu ya suala hili nakutana na mmoja wa wataalamu wa vifaa vya kuzimia moto  kutoka jeshi la zimamoto na uokoaji hapa anaelezea ni kwa namna gani wanatoa elimu kwa jamii juu ya matumizi ya vifaa hivyo.

Sauti ya mtaalamu wa vifaa vya kuzimamoto.