Dodoma FM

Matumizi ya Teknolojia yatajwa kuwa changamoto kwa watu wenye ulemavu

21 June 2022, 2:28 pm

Na;Mindi Joseph.

Watu wenye ulemuvu wametajwa kukabiliwa na changamoto katika matumizi ya Teknolojia ya Mitandao Licha ya kuendelea kufanya jitihada za kuhakikisha wanawasaidia.

Akizungumza na Taswira ya Habari Mkurungezi wa Taasisi ya zaina Foundation Zaituni Njovu amesema wanaendelea kuhakikisha kundi la watu wenye ulemavu wanawasaidia katika kuhakikisha wanawezesha katika matumizi ya mitandao.

Ameongeza kundi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali katika matumizi ya teknolojia ya Mtandao.

.

Katika hatua nyingine amesema wanatoa elimu na wanatarajia katika siku zijazo watu wenye ulemavu watanufaika na matumizi ya mitandao ya Kijamii.

.

Aidha wamewaomba wadau na serikali kuendelea kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kutengeneza njia rafiki ambazo zitawawezesha watu wasiioona na Viziwi waweze kutumia mitandao ya kijamii kwa urahisi.