Dodoma FM

Nzuguni A waishukuru Serikali kwa kuchonga barabara

28 March 2024, 7:36 pm

Wananchi wa mtaa huu wamepongeza kuanza kwa ukarabati huu ambao unaondoa hali mbaya iliyokuwepo mwanzo ikiwemo kujaa maji .Picha na George John.

Ni msimu wa kiangazi tu Barabra hii ilikuwa inapitika Lakini Msimu wa masika ilikuwa ni kikwazo.

Na Mindi Joseph.

Wakazi wa Nzuguni A wameishukuru Tarura kwa Uchongaji wa barabara Kilometa 9.780 na uzibaji wa mashimo kwa kifusi katika mtaa huo ambao msimu wa mvua ilikuwa haipitiki kwa kugeuka kuwa Korongo.

Wananchi wa mtaa huu wamepongeza kuanza kwa ukarabati huu ambao unaondoa hali mbaya iliyokuwepo mwanzo ikiwemo kujaa maji na kuwapa ugumu wa Kuvuka.

Sauti za Wananchi wa mtaa huo.
Picha ni Barabara hiyo ambayo imeanza kukarabatiwa .Picha na George John.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Nzuguni A Onaely Mbatiani anasema uwekaji wa Culvert na ujenzi wa mtaro utagharimu milion 45.

Sauti ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Nzuguni A Onaely Mbatiani.

Uchongaji wa barabara na uzibaji wa mashimo kwa kifusi utagharimu sh Milion 23 na ukarabati huu utakamilika tarehe 30 June.