Dodoma FM

Polisi waomba ushirikiano wa viongozi wa dini kufichua ukatili

27 July 2026, 16:40

Picha ni Jeshi la poliosi Tanzania baada ya kutoa elimu kwenye kanisa hilo.

Mrakibu Mnyanyi amebainisha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi hivyo utekelezaji wake unahitaji ushirikiano wa kila mmoja.zilizosaini mikataba ya kikanda na kimataifa ya kupinga ukatili wa kijinsia,

Na Stephen Noel.

Jeshi la Polisi Tanzania limewaomba viongozi wa dini pamoja na jamii kushirikiana katika kufichua matukio ya ukatili wa kijinsia ili kujenga jamii isiyo na ukatili.

Wito huo umetolewa na Mrakibu wa Polisi Mnyanyi wakati akitoa elimu ya ukatili katika Kanisa la Roman Katoliki, Parokia ya Bikira Maria wa Fatima, Mpwapwa.

Amesema Jeshi la Polisi kutoka mikoa yote limeungana na kusambaa mitaani na kwenye nyumba za ibada kutoa elimu ya ukatili kwa lengo la kupunguza vitendo hivyo. Pia ni kuwapa jamii nafasi ya kuripoti matukio hayo kwa wakati.

“Siku hadi siku kunakuwa na masuala ya ukatili yanayoripotiwa. Lakini wengine wamekuwa wakifanyiwa matendo hayo bila kujua hatua za kuchukua pindi wanapofanyiwa vitendo hivyo” amesema.

Ameongeza: “Ukatili kwa sasa hauna jinsi wala eneo. Kila mahali hutokea. Ni jukumu la kila mmoja kutoa taarifa za ukatili ili zifanyiwe kazi na kupunguza madhara ya ukatili.”

Sauti ya Noel