Wakulima wanaweza kupokea malipo ya mazao kupitia Mixx by Yas
7 August 2026, 20:17

Hii ni hatua inayolenga kuboresha ukusanyaji wa mapato ya wakulima, kuongeza upatikanaji wa mikopo ya kilimo na kulinda afya ya mifugo kupitia bima, yote kwa njia yenye usalama na ufanisi kupitia simu zao za mkononi.
Na Anwary Shabani.
Wakulima mkoani Dodoma wamehimizwa kutumia huduma za kifedha kidijitali zinazotolewa na Mixx by Yas ili kurahisisha upokeaji wa malipo ya mazao, kupata mikopo na kufanya miamala kwa usalama.
Meneja wa Biashara wa Mixx by yas kanda ya kati Bw.Charles Gasper ametoa wito huo wakati wa maonesho ya nane nane yanayoendelea jijini Dodoma Bw,Gasper amesema kupitia huduma ya Mixx kilimo,Wakulima wanaweza kupokea malipo ya mazao moja kwa moja kupitia simu , kupata mikopo ya pesa hadi shilingi milioni tatu.
Kwa upande wake, Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Dodoma, Joseph Chitinka, amesema ushirikiano kati ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Ushirika na Mixx by Yas umeongeza matumizi ya malipo ya kidijitali kwa wakulima na vyama vya ushirika mkoani humo.
Aidha, huduma za Mixx zimesaidia vyama vya ushirika na SACCOS kufanya miamala kwa urahisi, aidha Mrajis Msaidizi amewapongeza kwa mchango wao katika kuimarisha ujumuishaji wa huduma za kifedha kidijitali kwa wakulima na wanachama wa vyama vya Ushirika.