Dodoma FM
Dodoma FM
8 August 2025, 3:15 pm

Awali wangombea walijinadi kwa kutaja Majina pamoja na namba kutokana na majina yao.
Na Kitana Hamis.
Wajumbe walio shiriki Uchaguzi wa Udiwani kata ya Engusero Wilayani Kiteto walalamika kubadilishiwa namba za wagombea na kujikuta wakiwapigia kura wagombea wengine.
Wakizungumza Baadhi ya Wajumbe walio shiriki Uchanguzi wa Udiwani kata ya Engusero Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, Wamesema awali wangombea walijinadi kwa kutaja Majina pamoja na namba kutokana na majina yao, nabadala yake wamejikuta wakiwapigia watu wengine kwa kubadilishwa namba hizo.
