Dodoma FM

Wananchi watakiwa kutoa taarifa za majanga ya moto haraka

5 May 2025, 6:32 pm

Picha ni askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji wakiwa katika maadhimisho hayo.Picha na Kitana Hamis.

Siku ya Zimamoto Duniani huadhimishwa kila May 4 ya kila mwaka.

Na Kitana Hamis.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Mkoa wa Manyara Gilbert Mvungi,ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa mapema pindi ajali ya moto inapotokea kwakupiga namba ya dharura 114, akisisitiza kuwa hatua hiyo inaweza kuokoa maisha na mali.

Akizungumza wakati wa matembezi yakuhamasisha jamii kuhusu kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto, yaliyofanyika katika mitaa mbalimbali ya Mji wa Babati ikiwa nisiku ya maadhimisho ya Zimamoto Duniani Mei4, Mvungi alisema ushirikiano wa wananchi ninguzo muhimu katika jitihada za kupunguza athari za moto.