Wakulima wa Zabibu Handali walia na changamoto ya soko la uhakika
21 May 2026, 17:44

Licha ya changamoto ya wanunuzi wa zabibu msimu wa mavuno pia wanaiomba serikali kuwapatia bora kwa bei nafuu ili waweze kuzalisha zabibu zenye ubora.
Na Victor Chigwada.
Wakulima wa zabibu katika Kata ya Handali wilayani Chamwino wameiomba Serikali kutatua changamoto ya masoko ya zao Hilo pamoja na utoaji wa mbegu Bora Kwa bei nafuu.
Wakiongea na Taswira ya habari wakulima hao wamesema licha ya juhudi wanazo zifanya wakati wa kilimo unapokuja msimu wa mavuno wanakosa soko la uhakika la kuuzia zao hilo hivyo wanajikuta wanauza zabibu bila mpangilio mzuri wa bei.
Aidha wamesema licha ya changamoto ya wanunuzi wa zabibu msimu wa mavuno pia wanaiomba serikali kuwapatia bora kwa bei nafuu ili waweze kuzalisha zabibu zenye ubora na zinazo weza kukidhi soko la kimataifa.
Mwenyekiti wa maendeleo Kata ya Handali Bw.Emmanuel Madali amekiri wakulima wa eneo hilo kukabiliwa na changamoto ya soko msimu wa mavuno lakini tayari serikali ina mpango wa kujenga kiwanda katika eneo hilo ambapo wakulima watauza zabibu zao kwa urahisi zaidi kiwandani hapo.