Dodoma FM

Wakulima wasisitizwa umuhimu wa mfumo wa stakabadhi ghalani

18 June 2026, 18:07

Picha ni mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh.Rosemery  Senyamule alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Dabalo.Picha na Mkoa wa Dodoma.

Katika hatua nyingine, Mhe. Senyamule amewaahidi wakulima kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi yatakayowasaidia kukuza na kuimarisha sekta ya kilimo.

Na Mariam Kasawa.

Wakulima wa kata ya Dabalo jijini Dodoma waamesisitizwa umuhimu wa matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani kwa wakulima.

Wito huo umetolewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh.Rosemery  Senyamule alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata hiyo .

Mmoja ya wananchi waliokuwa katika mkutano huo, alilalamikia mfumo huo akieleza kuwa unachelewesha malipo ya wakulima wa zao la ufuta pamoja na bei kuwa chini ikilinganishwa na matarajio yao.

Sauti ya Mkulima.

Akijibu hoja ya bei kubwa, Mhe. Senyamule amewataka wakulima kuwa wavumilivu pindi yanapotokea mabadiliko ya bei za mazao kwani baadhi ya mazao, ikiwemo ufuta hutegemea hali ya soko la Kimataifa.

Sauti ya Mhe. Senyamule