Dodoma FM
Dodoma FM
10 October 2025, 11:33 am

Aidha, amebainisha kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kuhakikisha kuwa viwanda hivyo vinarejea katika hali ya uzalishaji ili kuimarisha uchumi wa wananchi wa Rungwe na kuongeza tija katika sekta ya kilimo cha chai nchini.
Na Selemani Kodima.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli, amewatoa hofu wafanyakazi wa zamani wa Viwanda vya Chai vya Tumba na Mwakaleli vilivyopo Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya, waliositishiwa ajira bila kulipwa stahiki zao, kwa kuwahakikishia kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha wanapata haki zao stahiki.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo jijini Dodoma, Bw. Mweli ameeleza kuwa Serikali inatambua changamoto zilizowakumba wafanyakazi hao na tayari imeanza kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha haki zao zinalindwa.
Aidha, amebainisha kuwa serikali inaendelea na mchakato wa kuhakikisha kuwa viwanda hivyo vinarejea katika hali ya uzalishaji ili kuimarisha uchumi wa wananchi wa Rungwe na kuongeza tija katika sekta ya kilimo cha chai nchini.
Katika hatua nyingine, Bw. Mweli amesisitiza kuwa Wizara ya Kilimo itaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wote kuhakikisha kuwa sekta ya chai inaimarika na kuwa chanzo kikuu cha mapato kwa wakulima na taifa kwa ujumla.