Dodoma FM

Umbali wakwamisha vijana kufuatilia vitambulisho vya NIDA

24 March 2026, 17:12

Umbali wa kufuatilia vitambulisho vya Taifa umewakatisha tamaa wengi ambao hawana vitambulisho. Picha na Mtandao.

Aidha wameongeza kuwa umbali wa kufuatilia vitambulisho vya Taifa umewakatisha tamaa wengi ambao hawana vitambulisho hivyo ikiwemo vijana na kubaki bila vitambulisho vya Taifa.

Na Victor Chigwada.

Vijana wa kata ya Ngh’ambaku wilayani chamwino ambao hawana vitambulisho vya Taifa NIDA wametakiwa  kufika katika mamlaka ya vitambulisho ili kupata vitambulisho hivyo.

Akizungumza na taswira ya habari afisa maendeleo ya Kata ya Ngh’ambaku Bw.Richad Kisubi amesema vijana wengi wa eneo hilo hawana vitambulisho vya Nida jambo linalo wapelekea vijana hao kukosa fursa mbalimbali.

Sauti ya Bw.Richad Kisubi.

Nao baadhi ya wananchi wa Kata hiyo wamesema kuwa ufuatiliaji wa namba za NIDA umekuwa mgumu kwao kwani wanalazimika kusafiri umbali mrefu kutoka kijijini hapo hadi Dodoma mjini ili kupata vitambulisho vya Nida.

Sauti za wananchi.