Dodoma FM

Shule ya msingi Iboni yawezeshwa ujenzi wa mabweni

7 February 2024, 5:29 pm

Picha ni Mabweni hayo ambayo yanajengwa katika shule ya Msingi Iboni .Picha na Nizar Mafita.

Shule ya msingi Iboni ni shule pekee mkoani dodoma inayotoa elimu ya kawaida na elimu ya vitengo maalumu wakiwemo wanafunzi wasiiona, viziwi, usonji na ulemavu wa akili na viungo huku baadhi yao wakitembea umbali mrefu kufika shuleni.

Na Nizar Mafita.
Shule ya Msingi Iboni iliyopo wilayani Kondoa mkoani Dodoma imewezeshwa ujenzi wa mabweni ya watoto wenye uhitaji maalumu kwa ajili ya kuwarahisishia haki ya kupata elimu hasa kwa watoto wenye usonji na wasioona.

Baada ya changamoto ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu kushindwa kusoma kwa kuishi mbali na shule ya msingi iboni

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi iboni mwalimu Fabian Charles akizungumza na amesema ufadhili wa ujenzi wa mabweni hayo unagharimu fedha kiasi cha shilingi milioni 270,934332

Sauti ya mwalimu Fabian Charles.
Shule hiyo inasema ujenzi wa mabweni hayo utawarahisishia wanafunzi. Picha na Nizar Mafita.

Mwalimu charles amesema kukamilika kwa mabweni hayo kutarahisisha elimu kwa watoto wenye mahitaji maalumu waishio wilayani kondoa.

Sauti ya mwalimu Fabian Charles.

Mwalimu Adam Awadhi kutoka kitengo cha ulemavu wa akili na usonji ameeleza kuwepo kwa changamoto ya darasa la wanafunzi wenye ulemavu wa akili pamoja na kuwepo kwa wastani wa walimu wa watoto wenye usonji.