Dodoma FM

Wasomi watakiwa kuwa mfano upandaji wa miti

26 March 2024, 8:11 pm

Picha ni mmoa kati ya wanafunzi wa Chuoa alie shiriki katika zoezi la upandaji miti .Picha na Noah Patrick

Hapa nchini kampeni nyingi za upandaji miti zimekuwa zikianzishwa na kutekezwa na wadau mbalimbali pamoja na wadau wa mazingira ili kuunga mkono juhudu za raisi wa Tanzania mama Samia Suluhu za kutaka mazingira Bora kwa wananchi.

Na Mariam Kasawa.
Wasomi na wanafunzi wa vyuo wametakiwa kutambua kuwa jukumu la kutunza mazingira linawahusu kwa kiasi kikubwa.

Hii ni kufuatia kampeni ya msomi na Tanzania ya kijani ambayo inatekelezwa katika vyuo mbalimbali hapa nchini kwa kupanda miti katika maeneo yanayo wazunguka na maeneo ya wazi.

Miti ni uhai na chanzo cha hewa Safi katika mazingira. Picha na Mariam Kasawa.

Je kampeni hii imefanikiwa kwa kiasi gani? Nimezungumza na baadhi ya wanafunzi walio shiriki kupanda miti katika bonde la makutupora wao walikuwa na haya ya kusema.

Sauti za wanafunzi wa chuo.

Miti ni uhai na chanzo cha hewa Safi katika mazingira wadau wa mazingira wanasema wasomi wanapaswa kuwa chachu na mfano wa kutunza mazingira na kupanda miti kwa Wingi .

Sauti ya Mdau wa Mazingira