Dodoma FM

Wakazi wa Njoge waishukuru serikali kwa kuboresha sekta ya elimu

19 October 2022, 9:29 am

Na ;Victor Chigwada.  

Wananchi wa Kata ya Lenjulu Wilaya ya Kongwa wametoa shukrani zao kwa Serikali ya awamu ya sita kwa jitihada za kuendelea kuboresha sekta ya elimu nchini

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamepongeza jitihada hizo za Serikali  kwani wamefanikiwa kujenga vyumba vya kujitosheleza katika shule ya sekondari lenjuru

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lenjuru Bw.Enock Mahungo amesema kuwa hapo awali walikuwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya maabara na madarasa lakini kwasasa changamoto hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa

.

Aidha Diwani wa kata hiyo Bw.Brown Chisongela amesema kuwa kutokana na fedha walizopatiwa na Halmashauri zimeleta Chachu ya  kukabiliana na changamoto ya madarasa,matundu vya vyoo na vyumba vya masomo ya sayansi

.

Mikakati ya kuongeze kwa vyumba vya madarsa imekuwa kipaumbele katika   shule mbalimbali  nchi ikiwa Ni hatua ya kukabiliana na changamoto ya ongezeko la wanafunzi