Dodoma FM

Uchangiaji wa vifaa vyenye ncha kali watajwa kuchangia maambukizi ya homa ya ini

21 February 2022, 3:32 pm

Na; Benard Filbert.

Imeelezwa kuwa kuchangia matumizi ya vifaa vyenye ncha kali ni miongoni mwa sababu zinazoweza kupelekea ugonjwa wa ini.

Hayo yameelezwa na daktari bingwa wa magonjwa ya figo kutoka Hospital ya Benjamin Mkapa Bwana Festo Sizamin wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu ugonjwa wa ini.

Amesema jamii inatakiwa kutambua ugonjwa wa ini ni miongoni mwa magonjwa  hatari ambao unasababishwa kwa njia tofauti ikiwa ni pamoja na kuchangia vifaa vyenye ncha kali.

Amesema njia pekee ya kuzuia ugonjwa huo ni kuongeza uelewa kwa jamii namna ambavyo ugonjwa huo unasambaa hali itakayosaidia kuzuia.

Baadhi ya wananchi wamezungumza na taswira ya habari wamesema hawana elimu ya kutosha kuhusu ugonjwa huo hivyo elimu iendelee kutolewa.

Ugonjwa wa ini ni miongoni mwa magonjwa hatari hivyo jamii inatahdharishwa kuchukua hatua mapema kabla ya kuambukizwa.