Dodoma FM

Maadhimisho ya muungano kufanyika Dodoma April 26

21 April 2022, 10:43 am

Na; Selemani Kodima.

Serikali imesema kuwa maadhimisho ya miaka 58 ya muungano wa Tanzania yanatarajia kufanyika tarehe 26 April 2022 jijini dodoma ambapo Mgeni Rasmi atakuwa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan.

Taarifa  iliyotolewa leo ya maadhimisho ya sherehe za kutumiza miaka 58 ya muungano wa tanganyika na Zanzibar  kupitia kwa Mawaziri watatu  ambao ni waratibu moja kwa moja wa sherehe hizo ambao ni Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais(Muungano na Mazingira ),Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera ,Bunge na Uratibu )na  Waziri wa ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi .

Akizungumza juu ya maandalizi ya hayo Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera ,Bunge na Uratibu )Mh George Simbachawene Amesema maadhimisho hayo yanatarajia kuhudhuriwa na wageni mbalimbali kuanzia Juma hili mpaka Kilele chake April 26.

.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Seleman Jafo amesema maadhimisho ya muungano ya Mwaka huu yataambatana na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuelimisha umma kuhusu tulipo toka,tulipo na tunapoelekea

.

Aidha kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe, Hamza Hassan Juma  ametoa wito kwa watanzania kiujumla kushiriki katika shamra shamra za maadhimisho ya hayo kwa kufanya shughuli za kijamii .

.

Tarehe 26 Aprili 1964, Tanganyika iliugana na Zanzibar na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo shughuli mbalimbali zinatarajiwa kufanyika katika maadhimisho ya mwaka huu ambapo ni Miaka 58 Tangu Kuasisiwa kwa Muungano wa Tanzania.