Dodoma FM

Serikali yaanza kudhibiti ndege waharibibu Bahi

29 March 2023, 5:38 pm

Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe akizungumza na wananchi . Picha na Fred Cheti.

Na Fred Cheti.

Serikali wilaya Bahi imesema tayari imeshaanza kuchukua hatua ili kuwaangamiza ndege hao.

Ndege hao aina ya Kwerea Kwerea wanaoharibu mazao katika vijiji vya Lukali,Mundemu ,Mayamaya na Zanka vilivyopo wilayani Bahi.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe wakati alipokua katika ziara ya kutembelea katika vijiji hivyo kuona namna ambavyo ndege hao wamefanya uharibu katika mashamba ya wakulima katika vijini hivyo ambapo ameelezea mikakati iliyopo katika kuwaangamiza ndege hao waharibifu.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe

Mheshimiwa Gondwe amewataka wakulima wilaya humo kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo suala hilo linashughulikiwa licha ya usumbufu mkubwa wanaopata kutokana na uharibufu unaofanywa na ndege hao.