Dodoma FM

Taka, chupa za plastiki ni mali katika mazingira

5 February 2024, 6:02 pm

Picha ni taka za plastiki pamoja na chupa zikiwa zimekusanywa eneo moja baada ya kununuliwa kutoka kwa watu wanao kusanya taka hizi mtaani. Picha na Mariam Kasawa.

Kwa mujibu wa redio Vatican inasena chupa za plastiki ambazo zilipaswa kutumika tena, lakini sehemu kubwa ya shehena za chupa inaishia kuwa ni taka zinazoendelea kutupwa na hivyo kuhatarisha maisha ya watu wengi duniani chupa hizi kamwe hazitaoza na zitaendelea kuwa ni sehemu ya kero na uchafuzi wa mazingira.

Na Mariam Kasawa.
Wananchi watakiwa kutambua kuwa taka za plastiki zinaweza kuleta manufaa na kuongeza vipato vya familia endapo zitatuzwa na kupelekwa mahali sahihi.

Katika Jiji la Dodoma biashara ya chupa za plastiki inaonekana kushamiri katika maeneo machache huku taka nyingi za plastuki pamoja na chupa zikichanganywa na taka zingine zinazo zalishwa majumbali na kutupwa katika dampo mbalimbali bila kujali faida zake.

Kuna methali moja walinena wahenga Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno lakini watu wanao jihusisha na uokotaji wa chupa hizi wanalalamika kukutana na changamoto mbalimbali katika kaya za watu je ni zipi hizo.

Sauti ya muokota Chupa.
Picha ni taka za plastiki pamoja na chupa zikiwa zimekusanywa eneo moja baada ya kununuliwa kutoka kwa watu wanao kusanya taka hizi mtaani. Picha na Mariam Kasawa.

Umekwisha wahi kujiuliza endapo taka hizi za plastiki zitasuswa mtaani kwa wiki mbili bila kuokotwa nini kitatokea Bw. Masesa ni mnunuzi wa chupa za plastiki katika mtaa wa Wajenzi Jijini Dodoma hapa anaeleza zaidi kuhusu biashara hii.

Sauti ya mnunuzi wa Chupa.

Isaya Silungwe ni Mkurugenzi wa mtendaji wa asasi ya Youth Forum inayo jihusisha na utunzaji wa nazingira yeye anasema taka za plastiki zikitunzwa vizuri zinaweza kusaidia kumuongezea mtu kipato.

Sauti ya Isaya Silungwe.