Dodoma FM

Adha ya maji Matumbulu kuwa Historia

18 December 2020, 3:52 pm

Na, Benard Filbert,

Dodoma.

Ili kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji katika Kata ya Matumbulu Mkoani Dodoma Serikali imeelekeza nguvu zake katika kutatua adha hiyo ili kuleta unafuu kwa wananchi.
Akizungumza na taswira ya habari afisa mtendaji wa Kata hiyo Bw.Stanley Motambi amesema Serikali imejitahidi kwa kiasi kikubwa kutafuta vyanzo vya maji ili kuondoa kero hiyo ambayo inakwamisha shughuli nyingine za uzalishaji kwa wananchi kupoteza muda mwingi.
Amesema mpaka sasa katika Kata ya Matumburu kuna visima viwili ambavyo vinatoa maji lakini wanasubiri kukamilika kwa miundombinu ya umeme wa REA ambao utasaidia kuvuta maji kwenye visima vilivyochimbwa.

Kadhalika amesema kisima kingine kimechimbwa katika mtaa wa ukombozi ambacho kitarahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi pamoja na wanafunzi ambao walikuwa wakilalamika kwa kiasi kikubwa kuliko maeneo mengine.

Moja kati ya visima vya kisasa vinavyojengwa

Kukosekana kwa huduma ya maji katika baadhi ya maeneo kunarudisha nyuma maendeleo kwani baadhi ya shughuli hazifanyiki kutokana na kukosa maji.