Dodoma FM

Ihumwa waomba kuboreshewa soko

26 March 2021, 9:49 am

Na; Shani Nicolaus.          

Wafanyabiashara  katika Mtaa wa Ihumwa jijini Dododma wametoa wito wa kukarabatiwa soko lao ili waepukane na changamoto wanayokumbana nayo hasa msimu wa mvua.

Wakizungumza na Dodoma fm wafanyabiashara hao wameomba kutatuliwa adha hiyo mara baada ya kukamilika kwa shughuli ya kumpumzisha aliyekuwa rais wa awamu ya tano hayati Dkt.John Magufuli.

Wamesema kuwa wapo tayari kushirikiana na Serikali katika ukarabati wa soko hilo hivyo wanaiomba iwawekee utaratibu mzuri wa kuuanza ujenzi huo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Mtaa wa Ihumwa A  Bw.William Njilimuyi amesema mpango wa kukarabati soko hilo upo, hivyo kuna pesa inasubiriwa  kutoka shirika la reli  baada ya ujenzi wa reli ya mwendokasi kupitia katika maeneo yao na  mara baada ya kumaliza maombolezo ya hayati Dkt Magufuli wataanza kufuatilia fedha hizo.

Amesema bado wafanyabiashara  wa Ihumwa wanaenzi kauli ya hayati Dkt.Magufuli ya hapa kazi tu, kwa kuchapa kazi kwa bidii.