Dodoma FM

Wahitimu BBT kwenda JKT mafunzo ya uzalendo

28 July 2023, 4:21 pm

Waziri wa Kilimo Hussen Bashe alipotembelea shamba la   BBT Ndogowe lililopo wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma. Picha na Wizara ya Kilimo.

Mnamo Tarehe 23 Februari, 2023 serikali kupitia Wizara ya Kilimo ilitangaza awamu ya kwanza ya majina 812 ya vijana waliochaguliwa kujiunga katika programu ya Building Better Tomorrow: Youth Initiative in Agribusiness (BBT-YIA). Serikali kupitia programu hii itawawezesha vijana kushiriki kilimo biashara kupitia mashamba makubwa( BLOCK FARMING)

Na Fred Cheti.

Waziri wa Kilimo  Mhe Hussein  Bashe amesema  kuwa vijana wanaomaliza mafunzo ya BBT mwezi Agosti watakwenda JKT kwa ajili ya mafunzo ya uzalendo kabla ya kupelekwa mashambani.

Waziri Bashe ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea shamba la   BBT Ndogowe lililopo wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma ambapo ameongeza kuwa mchakato ujao wa kuwapata washiriki wa mafunzo hayo ya BBT Wizara ya kilimo  itashirikiana na JKT kwa awamu zote zinazofuata ili kupata vijana wazalendo .

Sauti ya waziri wa kilimo.

Akizungumzia kuhusu shamba hilo la Ndogowe ambalo ni moja kati ya mashamba ambayo yatapokea vijana wanaomaliza mafunzo ya BBT mwezi Agosti, Waziri Bashe amesema:

Sauti ya waziri wa kilimo.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akizungumza alipotembelea shamba hilo la BBT. Picha na Wizara ya Kilimo.

Kwa upande wake Bwana Prsosper Makundi ambaye ni mkuu wa kitengo cha mazingira kutoka Wizara ya Kilimo amesema kuwa kilimo kitakachokuwa kikifanyika katika mashamba hayo kitazingatia sheria zote za utunzaji wa mazingira.

Sauti ya Mkuu wa kitengo cha mazingira.