Dodoma FM

Umwagaji wa mafuta machafu hovyo huchangia kuharibika kwa barabara

13 January 2022, 2:32 pm

Na; Thadei  Tesha.

Imeelezwa kuwa miongoni mwa ajali zinazotokea mara kadhaa nchini baadhi ya ajali hizo zinatokana na umwagaji wa mafuta machafu hovyo na kusababisha kuharibika kwa miundombinu ya  barabarani.

Baadhi ya madereva pamoja na watembea kwa miguu jijini hapa wamesema ni wakati wa mamlaka husika kuhakikisha zinatoa elimu kwa wananchi juu ya athari za umwagaji mafuta kiholela hovyo hususani barabarani ili kupunguza kuharibika kwa barabara ikiwa ni pamoja na uchafuzi wa mazingira.

Aidha uwepo wa gereji bubu ambazo zimekuwa zikianzishwa kiholela na baadhi ya mafundi hao wametajwa kama miongoni mwa kundi linalohusika kwa wingi kumwaga mafuta kiholela pamoja na uchafuzi wa mazingira.. 

Akizungumzia suala hilo ofisini kwake jijini hapa afisa mazingira wa jiji la dodoma amewataka mafundi wa gereji kuzingatia utunzaji wa mazingira katika shughuli zao ambapo ametoa wito kwa gereji bubu za pikipiki na bajaji kufanyia shughuli zao katika maeneo yaliyotengwa.

Wataalamu mbalimbali wamekuwa wakisisitiza suala la utunzaji wa miundombinu ambapo umwagaji wa mafuta kiholela barabarani ni moja ya uharibifu wa barabara hizo.