Dodoma FM

Nigeria:Zaidi ya wanafunzi 300 hawajulikani walipo

14 December 2020, 3:26 pm

Abuja,

Nigeria.

Gavana wa Jimbo la Katsina la Nigeria Aminu Masari amesema, wanafunzi 333 bado hawajulikani walipo baada ya shambulizi lililofanywa usiku wa Ijumaa na watu wenye silaha katika shule moja ya sekondari katika jimboni Katsina, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Bw. Masari ameamuru shule zote za sekondari za bweni jimboni humo kufungwa.

Pia amesema idara za usalama zimechukua hatua na kuwasaka washambuliaji.