Dodoma FM

Huduma za kijamii zazidiwa na ongezeko la watu

10 February 2023, 1:45 pm

picha inayo onyesha baadhi ya makazi na huduma za jamii. Picha na wikimedia.

Waziri wa Nishati na Madini Januari Makamba mwaka jana dec 25 alisema kuwa  Wizara inaanza program ya kupeleka umeme kwenye vitongoji. Kwani tayari serikali imefikia asilimia 75 katika kufikisha umeme vijijini

Na Victor Chigwada.                                                         

Imeelezwa kuwa ongezeko la watu na ukuaji wa miji na vijiji hauendani na upatikanaji wa huduma za kijamii katika baadhi ya maeneo,

Hilo limefahamika baada ya Taswira ya habari kufanya mahojiano na Diwani wa Kata ya Mlowa barabarani Bw.Anjelo Lukasi  ambapo amesema kuwa pamoja na uwepo wa vitongoji ishirini katika kata yake lakini ni vitongoji saba tu ndivyo vyenye huduma ya nishati ya umeme

Hata hivyo Lukasi ameongeza kuwa tayari wamewasilisha maombi hayo sehemu husika na kupewa ahadi ya kutekelezewa huduma hiyo

Anjelo Lukosi

Naye menyekiti wa kijiji cha Mloda amesema kuwa licha ya vitongoji vichache kunufaika na nishati ya umeme lakini idadi kubwa bado havija fikiwa hali ambayo ameiomba serikali   kuwakamilisha baadhi ya huduma

mwenyekiti