Dodoma FM

Ujenzi wa kituo cha Afya Mlowa barabarani kupunguza adha ya akina mama kujifungulia nyumbani

14 November 2023, 4:21 pm

Kukosekana kwa huduma za afya iliwalazimu akina mama kujifungulia nyumbani na kuhatarisha maisha yao.Picha na Google.

Pamoja na uwepo wa Hospitali hiyo ya wilaya lakini bado wana mikakati ya kuboresha zahanati katika kijiji cha Mlodaa.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa Kata ya Mlowa Barabarani Wilayani Chamwino wamesema ujenzi wa kituo cha afya ndani ya Kata yao utawasaidia kurahisisha huduma za afya ambazo walizikosa kwa kipindi kirefu.

Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa kutokana na kukosekana kwa huduma za afya iliwalazimu akina mama kujifungulia nyumbani na kuhatarisha maisha yao.

Sauti za wananchi.

Nae Mwenyekiti wa kijiji cha Mloda amekiri kwasasa licha ya uhafifu wa huduma za afya kijijini kwke lakini wananchi wamepata unafuu kupitia ujenzi wa kituo cha afya Mlowa barabarani

Sauti ya Mwenyekiti wa Mlodaa.

Diwani wa Kata hiyo ameipongeza Serikali kwa kuwapa fursa ya Hospitali ya Wilaya kujengwa ndani ya Kata yake na hivyo kupunguza adha ya huduma za afya

Sauti ya Diwani.

Ameongeza kuwa pamoja na uwepo wa Hospitali hiyo ya wilaya lakini bado wana mikakati ya kuboresha zahanati katika kijiji cha Mloda

Sauti ya Diwani.