Dodoma FM

Wakazi wa Chididimo waiomba serikali iwatatulie kero ya upungufu wa walimu

9 February 2022, 3:51 pm

Na; Neema Shirima.

Wakazi wa mtaa wa Chididimo kata ya Zuzu wameiomba serikali iwaongezee waalimu katika shule iliyopo katika mtaa huo.

Wakizungumza na taswira ya habari wananchi hao wamesema katika shule ya msingi Chididimo waalimu ni wachache jambo ambalo linawafanya wanafunzi washindwe kusoma masomo yao kwa wakati hivyo kuiomba serikali iweze kuwaongezea waalimu shuleni hapo

Aidha mwenyekiti wa mtaa huo bwana Boniface Laurent amekiri kuwepo changamoto ya upungufu wa waalimu shuleni hapo ambapo amesema kuwa shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya mia saba na waalimu saba ambapo uhitaji wa waalimu bado ni mkubwa

Amesema pamoja na upungufu wa waalimu bado shule hiyo inafanya vizuri na ufaulu wake umeongezeka kwa wanafunzi waliofaulu kujiunga na elimu ya sekondari lakini ameiomba serikali iwaongezee waalimu ili wanafunzi waweze kufanya vizuri zaidi

Ni jukumu la kila mzazi pamoja na serikali kuhakikisha watoto wanapata haki ya kupatiwa elimu kwani elimu ni msingi bora wa maisha yao ya baadae