Dodoma FM

Wadau watakiwa kufahamu mwongozo wa taifa wa wajibu wa wazazi, walezi

1 August 2023, 4:52 pm

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum wakili Amoni Mpanju amesema ni wajibu wa kila mmoja kulinda maadili ya kitanzania. Picha na wizara ya maendeleo ya jamii.

Mwongozo huo wa Malezi Bora umetokana na utafiti uliofanywa na serikali kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto duniani UNICEF, ambapo nguzo kuu tatu zitazingatiwa kwenye mwongozo huo za Kujali, Kulinda na Kuwasiliana na mtoto.

Na Mariam Kasawa.

Imeelezwa kuwa ili kufanikisha suala na malezi yenye kuzingatia maadili ya kitanzania na kuyalinda ni muhimu wadau mbalimbali kuungana pamoja na kufahamu muongozo wa taifa, wajibu wa wazazi na walezi kwa malezi ya familia wa mwaka 2023.

Naibu katibu mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalum wakili Amoni Mpanju amesema ni wajibu wa kila mmoja kulinda maadili ya kitanzania ili kuondokana na mmomonyoko wa maadili.

Sauti ya Naibu Katibu mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii
Imeelezwa kuwa ili kufanikisha suala na malezi yenye kuzingatia maadili ya kitanzania na kuyalinda ni muhimu wadau mbalimbali kuungana pamoja na kufahamu muongozo wa Taifa.Picha na UNICEF.

Akizungumzia lengo  la kukutana na viongozi wa dini, mkurugenzi idara ya watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Sebastiani Kitiku  amesema wameamua kuwashirikisha viongozi wa dini ili kupata sauti ya pamoja katika kulinda maadili.

Sauti ya mkurugenzi idara ya watoto kutoka wizara ya maendeleo ya jamii

Nao viongozi wa dini wamesema utandawazi umechangia kwa kiasi kikubwa mmomonyoko wa maadili na kuahidi kuwa mabalozi wazuri katika malezi ya watoto ili kupata taifa lenye maadili.

Sauti za viongozi wa Dini.