Dodoma FM

Utiririshaji wa maji taka waweka mashakani afya za wakazi wa mtaa wa Majengo

13 December 2023, 7:34 pm

Picha ni chemba inayotiririsha maji taka katika mtaa wa Majengo Jijini Dodoma. Picha na Khadija Ibrahim.

Ubovu wa miundombinu ya maji taka hasa kipindi cha masika inatajwa kuwa ni hatari kwa afya ya binadamu kutokana na kutiririka kwa maji taka ambayo huambatana na uchafu wa kila aina.

Na Khadija Ibrahim.

Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Majengo Jijini Dodoma wameeleza kusikitishwa hali ya mazingira ilivyo katika maeneo yao kufuatia baadhi ya chemba kutiririsha maji machafu huku wakihofia usalama wao.

Taswira ya habari imefika eneo hilo na kuzungumza na baadhi ya waathirika wa mazingira hayo ambapo wameiomba mamlaka husika kutatua changangamoto hiyo.

Sauti za baadhi ya wananchi.
Mazingira hayo yamekuwa hatari hususani kwa wafanyabiachara hasa wa chakula. Picha na Khadija Ibrahim.

Baadhi ya wafanyabiashara katika eneo hilo wamesema usalama wa afya zao na pamoja na wateja uko hatarini kutokana maji hayo kutiririka katika biashara zao tofauti zikiwemo za vyakula.

Sauti za baadhi ya wafanyabiashara.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Fatina Majengo bi. Maua Mbarouk amesema malalamiko hayo tayari alishayafikisha kwa uongozi lakini hadi sasa hayajafanyiwa utekelezaji.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Fatina