Dodoma FM

Vijana wajengewa uwezo kupitia shindano la usalama mtandaoni

22 April 2021, 10:23 am

Na; Mindi Joseph.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema itaendelea kuboresha mawasiliano bora na salama kwa watumiaji kufuatia idadi ya watumiaji wa mtandao kufika milioni 27.9 Desemba 2020 mwaka ulio pita.

Akizungumza wakati wa kufunga shindano la pili la masuala ya usalama wa Mtandao kwa mwaka 2021 Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano kanda ya kati Bw. Boniface Shoo amesema jamii kubwa ya watazania mijini na vijijini inatumia simu hivyo  kuchangia gharama za huduma ya mawasiliano kupungua kwa kiasi kikubwa.

Ameongeza mashindano ya usalama mtandaoni ni njia bora ya kupata vipaji chipukizi na kukuza uwezo unaoleta tija na usalama mtandaoni kufuatia teknolojia ya intaneti  kuleta mapindizu katika sekta mbalimbali.

Baadhi ya washiriki kutoka vyuo mbalimbali Nchini wameishukuru TCRA kwa kuandaa mashindano hayo ya usalama Mtandaoni kwani yamewasaidia kuongeza ujuzi Zaidi na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa matumizi sahihi ya mitandao.

Mashindano ya usalama mtandaoni yalianzishwa kwa misingi ya kuwajengea uwezo wataalamu wa TEHAMA na kuongeza uwezo wa kiufundi katika eneo la usalama mtandaoni , shindano hilo muhula wa pili lilifunguliwa Desemba mosi 2020 na kuhitimishwa January 2021 ambapo lilijumuisha jumla ya  washiriki 583 walio sajiliwa kutoka vyuo 25 na washiriki 50 ndio walifanikiwa kufika fainali ya shindano hilo na kukabidhiwa vyeti.