Dodoma FM

Mteremko mkali tishio kwa maafisa usafirishaji kisima cha nyoka

4 April 2023, 3:20 pm

Moja ya kona za mtaa huo wa kisima cha nyoka. Picha na Thadei Tesha.

Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa ni vyema serikali kuendelea kuboresha mazingira ya miundombinu ya barabara kutokana na umuhimu wake katika shughuli mbalimbali za kijaamii pamoja na kiuchumi.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya vijana wanaojihusisha na biashara ya kuendesha pikipiki maarufu kama maafisa usafirishaji katika mtaa wa kisima cha nyoka jijini dodoma wameiomba serikali kuboresha eneo la kituo wanachofanyia biashara zao ili kupunguza ajali za mara kwa mara ndani ya eneo hilo.

kutokana na uwepo wa mteremko mkali katika eneo hili linasababisha wao kutokufanya vyema biashara zao kwani mara kadhaa wamekuwa wakishuhudia ajali kama wanavyoeleza.

Sauti za maafisa usafirishaji.
Moja ya kona za mtaa huo wa kisima cha nyoka. Picha na Thadei Tesha.

Aidha wameiomba serikali kupitia TARURA kuweka alama za tahadhari katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na matuta ili kuepuka athari mbalimbali ikiwemo watu kupoteza maisha.

Sauti za maafisa usafirishaji hao.