Dodoma FM

Mradi wa maji wa Nzugumi wafikia asilimia 87

19 September 2023, 4:31 pm

Picha ni tanki la chuma la kukusanyia maji lenye ukubwa wa lita laki tano katika Mradi wa Maji wa Nzuguni jijini Dodoma .Picha Millard Ayo.

Mkoa wa Dodoma unazalisha nusu ya mahitaji ya maji ambapo mahitaji ya maji ni lita Milion 133 kwa siku na yanayozalishwa ni lita milion 67.8 hivyo kuwa na upungufu wa lita Milioni 66.7 kwa siku.

Na Mindi Joseph.

Mradi wa maji wa Nzuguni ambao unatarajia kukamilika mwanzoni mwa mwezi Oktoba umefika asilimia 87 ya utekelezaji wake.

mradi  huo ukikamilika utahudumia wananchi wa Nzuguni, Swaswa, Ilazo na Nyumba 300 wapatao 75,000.

Mkurugenzi  wa Usambazaji na Usafi wa Mazingira wa DUWASA, Mhandisi Emmanuel Mwakabole anazungumzia mradi huo.

Sauti ya Mhandisi Mwakabole.
Mradi huo umefikia asilimia 82 ambapo zaidi ya lita za maji milioni 7.6 zitazalishwa kwa siku, hivyo kuongeza asilimia 11 za upatikanaji maji katika Jiji la Dodoma.Picha na Millard Ayo.

Tenki la ujazo wa lita milioni tatu tayari limefungwa katika mradi mkubwa wa maji Nzuguni.

Sauti ya mhandisi Mwakabole.