Dodoma FM

Jamii imetakiwa kuichukulia siku ya valentine kuwa ni siku ya kuonyesha upendo kwa kila mtu

14 February 2022, 5:40 pm

Na; Benard Filbert.

Jamii imetakiwa kuacha dhana potofu kuwa siku ya wapendanao ni siku ya watu waliopo kwenye ndoa na badala yake siku hiyo itumike kuonesha upendo kwa kila mtu katika jamii.

Hayo janajiri kufuatia dhana iliyopo katika jamii asilimia kubwa ya watu kutumia siku hiyo kwa ajili ya kuonesha upendo kwa watu walionao kwenye mahusiano ya kimapenzi.

Paul luisulie ni mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dodoma amesema asilimia kubwa siku ya wapendanao imekuwa ikitumika tofauti na kusudio la siku hiyo jambo ambalo sio sawa.

Kadhalika amesema jamii inahitaji kuelimishwa kwa kiasi kubwa huku watu wakitakiwa kutumia siku hii kuonesha upendo wa kila aina.

Baadhi ya wananchi wamekiri kuwa siku hii kutumika kuonesha upendo wa aina moja kitu kinachosababishwa na kutokuwa na uelewa.

Kila tarehe 14 mwezi februari dunia inaadhimisha siku ya wapendanao lengo ikiwa kuonesha upendo kwa kila mwanandamu.