Dodoma FM

Mwarobaini vifo vya wajawazito Bahi wapatikana

24 July 2023, 2:04 pm

Jengo la zahanati ya kijiji cha Chali Igongo wilayani Bahi lililozinduliwa. Picha na Seleman Kodima.

Hatua hii ni muhimu ambapo takwimu zinazokusanywa katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini zinaonesha vifo vitokanavyo na uzazi vimeendelea kupungua kutoka vifo 1,640 mwaka 2020 hadi vifo 1,580 mwaka 2021.

Na Seleman Kodima.

Vifo vya akina mama wajawazito na watoto vinatarajiwa kuzidi kupungua wilayani Bahi kutokana na jitahada kubwa zinazofanywa na wadau kwa kushirikiana na serikali wilayani humo.

Hali hii imefahamika baada ya Dodoma FM kushuhudia uzinduzi wa zahanati katika kijiji cha Chali Igongo ambapo wananchi wa kijiji hicho wameelezea masaibu waliyokuwa wanayapitia hasa kwa akina mama wajawazito na watoto.

Sauti za wananchi.

Aidha hatua ya uzinduzi wa zahanati hiyo inaelezwa kuwa itasaidia kupunguza madhila wanayopitia wanawake hasa  vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi na watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano .

Zaina Mlawa ni Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Bahi akizungumza wakati wa makabidhiano ya zahanati hiyo ambayo imejengwa na wahisani wa Qatar Charity amesema kuwa amewashukuru wafadhili hao kwa moyo wao wa upendo kwa wananchi wa Bahi na kuahidi kuitunza zahanati hiyo

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Bahi.
Mwakilishi wa Qatar Charity Ahmed Elhamrawy akifungua jengo la zahanati hiyo. Picha na Seleman Kodima.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Bahi Mhe Keneth Nolo amesema hatua ya ujenzi wa zahanati hiyo  itawasaidia akina mama na watoto ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za kliniki.

Sauti ya Mbunge wa Bahi Mhe Keneth Nolo.

Naye mwakilishi wa Qatar Charity Ahmed Elhamrawy ameeleza haya juu ya hisani hiyo yenye kubeba matumaini ya wengi kutokana na umuhimu wa afya katika jamii.

Sauti ya Muwakilishi wa Qatar Charity Ahmed Elhamrawy.