Dodoma FM

Jumuiya za watumia maji Mpwapwa zatakiwa kuunganisha nguvu na serikali

27 June 2023, 5:08 pm

Kaimu mkuu wa wialaya ya Mpwapwa ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mh. Remidius Mwema akizungumza katika kikao hicho . Picha na Fred Cheti.

Amewataka watendeji kuendelea kusisitiza suala la utunzaji wa mazingira ili kuokoa vizazi vya sasa na vijavyo.

Na Fred Cheti.

Jumuiya za watumia maji katika halmsahuri ya wilaya ya Mpwapwa zimeaswa kuunganisha nguvu na serikali kwa kutoa ushirikiano utaokaosaidia kuundwa utaratibu mzuri utakaosaidiwa wananchi kupata huduma ya maji kwa urahisi.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Remedius Mwema wakati akichangia katika kikao kazi kilichokutanisha wataalamu wa maji,watendaji wa wilaya pamoja na wananchi ambao wanaunda jumuiya hizo za watumia maji kilichokua na lengo na kuutambulisha mfumo mpya ya ulipiaji maji.

Sauti ya Mh. Remidius Mwema.
Baadhi ya Wajumbe katika Mkutano huo. Picha na Fred Cheti.

Kwa upande wake Meneja wa Ruwasa katika halmashauri hiyo ya wilaya ya Mpwapwa Bwana Cyprian Warioba anaulezea Mradi wa EP4R yaani LIPA KWA MATOKEO mabao utakwenda kutumika kwa wananchi katika ulipiaji wa huduma za maji.

Sauti ya Meneja wa Ruwasa.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa halamshauri ya Mpwapwa ametumia fursa katika kikao hicho kuwataka watendeji kuendelea kusisitiza suala la utunzaji wa mazingira ili kuokoa vizazi vya sasa na vijavyo.

Sauti ya Mwenyekiti wa halamshauri ya Mpwapwa .