Dodoma FM

Wazazi watakiwa kusimamia Afya ya kinywa ya watoto wao

15 March 2022, 2:07 pm

Na;Yussuph Hassan.

Katika kuhakikisha Mtoto anapata makuzi bora ya afya ya kinywa, imeelezwa kuwa Mzazi ana wajibu wa kumsimamia Mtoto wake kuanzia umri wa Mwaka mmoja hadi kufikia umri wa miaka Tisa.

Usafi wa kinywa hujumuisha usafi wa meno, fizi, ulimi na eneo la juu mdomoni ambapo usafi huo endapo hautafanyika kwa umakini huweza kusababisha maradhi ya kinywa.

Mganga kutoka kliniki ya Kinywa na Macho Mkoani Dodoma (Shumahofa) Bw. Francis Mdoe amesema kuwa usafi wa kinywa kwa mtoto huanzia mara ya kuota meno.

Aidha bw. Mdoe amesema mswaki wa mtoto ni vyema ukazingatia umri wake ili kutoathiri ukuwaji wa menio na afya ya fizi.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya Wakazi Jijini hapa ambapo wameeleza kuwa suala la usafishaji wa kinywa kwa watoto ni changamoto inayohitaji elimu ya kutosha.

Kila ifikapo Machi 20 kila Mwaka dunia huadhimisha Siku ya afya kinywa lengo ni kukumbusha jamii juu ya kutunza na kupima magonjwa mbalimbali ya kinywa.