Dodoma FM

Serikali yatatua changamoto ya madarasa Membe

15 April 2021, 1:55 pm

Na; Benard Filbert.

Serikali katika Kata ya Membe Wilayani Chamwino imetatua changamoto ya madarasa iliyokuwa ikikwamisha wanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza 2021 kwa kujenga vyumba vya madarasa.

Hayo yameelezwa na diwani wa Kata ya Membe Bw.Simon Petro wakati akizungumza na taswira ya habari akielezea hatua zilizochukuliwa kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa.

Bw.Simon amesema kuwa tayari wanafunzi wameripoti shulenu baada ya awali vyumba vilivyokuwa vikitumiwa na walimu kubadilishwa matumizi kuwa madarasa kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi waliodahiliwa.

Kadhalika amesema kuwa  watoto ambao bado hawajaripoti ni wachache huku wengine ikielezwa wanakabiliwa na changamoto binafsi zikiwepo hali ngumu ya maisha.

Hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu zaidi ya wanafunzi 50 kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari Membe walikuwa hawajajiunga na masomo ya kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.