Dodoma FM

Zaidi ya wananchi 7000 watarajia kunufaika

9 February 2023, 10:30 am

Meneja wa Ruwasa wilayani Chemba wakati akitoa taarifa juu ya mradi huo.Picha na Martha Mgaya

Zaidi ya wananchi 7000 wa kijiji cha Ibihwa na Mpamantwa Wilayani Chemba wanatarajia kunufaika na huduma ya maji safi na salama pindi ujenzi wa mradi wa kisima kikubwa cha maji unaotekelezwa katika vijiji hivyo utakapokamilika.

Na Fred Cheti.

Mradi.Picha na Martha Mgaya

Hayo yameelezwa na Meneja wa Ruwasa wilayani humo wakati akitoa taarifa juu ya mradi huo mbele ya kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi ilipotembelea katika mradi huo unaotekelezwa kupitia fedha za Mfuko wa maji wa Taifa ili kujua maendeleo ya mradi huo.

Meneja wa Ruwasa Chemba.
Mradi.Picha na Martha Mgaya

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Bi. Pili agustino ameitaka mamlaka ya maji Ruwasa kuhakikisha inamsimia mkandarasi ili amalize maradi huo kwa wakati na uanze kutumika kwa ajili ya kurahisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi.

Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Bi. Pili Agustino