Dodoma FM

Fainali za CHAN 2021 Cameroon mambo yameiva

14 December 2020, 10:43 am

Younde,

Cameroon.

Waziri Mkuu wa Cameroon Dion Ngute akiwa na kaimu katibu mkuu wa CAF Baf Anthony Baffoe

Cameroon sasa wako tayari kuwa mwenyeji wa CHAN 2020 baada ya Kamati ya Utendaji ya CAF kuidhinisha miundombinu yake kutoka kwa ukaguzi wa mwisho ulioongozwa na Baf Anthony Baffoe, Naibu Katibu Mkuu anayehusika na mpira wa miguu na maendeleo.

Moja ya Viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya CHAN 2021 kikiwa tayari kwa matumizi

Rais wa kamati ya mawasiliano na habari za michezo Abel Mbengue,amesema katika hitimisho la ziara ya ukaguzi huo akiambatana na waziri mkuu wa nchi hiyo kuwa kwa namna hali ilivyo wameridhishwa na kasi ya maandalizi hivyo ni wazi CHAN itafanyika.

Michuano ya Total CHAN 2020 inatarajiwa kuanza 16 Januari hadi Februari 7 2021 ambapo Simba wasioshindika Cameroon watafungua dimba na Zimbabwe katika Uwanja wa Ahmadou-Ahidjo huko Younde.

Moja ya Viwanja ambavyo tayari vimekamilika