Dodoma FM

Asilimia 92 ya watumiaji wa mahakama nchini waridhishwa na huduma

19 May 2023, 4:38 pm

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma akizungumza na wafanyakazi wa Mahakama.Picha na Mindi Joseph.

Wafanyakazi wa mahakama wamejipambanua kwa kufanikisha na kusongeza huduma za utoaji haki karibu na wananchi.

Na Mindi Joseph.

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma amesema Asilimia 92 ya watumiaji wa mahakama wameridhishwa na utoaji wa huduma kutoka kwa majaji na mahakimu wa mahakama.

Takwimu hizi ni kwa mujibu ya utafiti uliofanywa na taasisi isiyo ya kiserikali REPOA Mwaka 2023 unaoonesha kuwa watumiaji hao walioneshwa heshima na uungwana kwa kila mmoja kutoka kwa majaji na mahakimu.

Prof. Ibrahim Juma ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Baraza kuu la wafanyakazi wa Mahakama Tanzania.

Sauti ya Prof. Ibrahim Juma.
Wafanyakazi wa Mahakama wakiwa katika Mkutano huo. Picha na Mindi Joseph.

Kamishna Msaidizi wa Kazi Bw. Andrew Mwalwisi amewahimiza wafanyakazi kutunza siri na nyaraka za serikali zinazohusu mhimili huo.

Sauti ya Kamishna Msaidizi wa Kazi.