Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuacha kutupa taka ovyo katika mazingira yao

4 September 2023, 3:27 pm

Mwenyekiti wa mtaa wa Kitenge kata ya Majengo Jijini Dodoma  Helswida Mhagama wakati akizungumza na Dodoma Tv. Picha na Diana Masai.

Serikali imekuwa ikikemea vitendo vya utupaji wa taka hovyo zikiwamo za plastiki lengo ni kuepusha uchafuzi wa mazingira unaotokana na taka hizo.

Na Diana Masai.

Ili kuondokana na uchafuzi wa mazingira jamii imeaswa kuacha kutupa  taka ovyo zikiwemo taka za plastiki ambazo haziozi.

Wito huo umetolewa na  Mwenyekiti wa mtaa wa kitenge kata ya Majengo Jijini Dodoma  Helswida Mhagama wakati akizungumza na Dodoma Tv ambapo  amesema ataendelea kushirikiana na viongozi wengine na pamoja na wananchi ili kutokomeza uchafuzi wa mazingira.

Sauti ya Bi. Helswida Mhagama.

Katika hatua Nyingine amewapongeza watu wanaojiari kupitia  shughuli ya uokotaji wa  makopo kwani husaidia juu ya utunzaji wa mazingira.

Sauti ya Bi. Helswida Mhagama.

Dodoma tv imekutana na Bwn. Maulidi  Juma ambaye  anajihusisha na upandaji wa miche mbalimbali  ya miti kwa kutumia makopo na hapa anatoa ushauri juu kwa wale wanaoshiriki kutupa makopo hayo bila utaratibu maalumu.

Sauti ya Bw. Maulid Juma.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi Jijini Dodoma wamesema kuwa wanaitambua sheria juu ya kosa la utupaji wa makopo hovyo na kuchangia uchafuzi wa mazingira na kushauri uongozi wa Jiji kushirikiana na jamii kwa karibu kutokomeza vitendo hivyo.

Sauti za baadhi ya wananchi.