Dodoma FM
26 June 2026, 15:01

Vijana wengi wakiwa wamehitimu vyuo na shule za ufundi bado wanakaa nyumbani bila kazi yoyote.
Na Steven Noel.
Ajira ni haki na fursa muhimu kwa kila raia, hasa vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa na ndio kundi kubwa lenye idadi ya watu , Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana imekuwa kubwa na inazidi kuongezeka.
Hali hii inapelekea vijana wengi kukata tamaa, umaskini na hata kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu na Msongo wa mawazo na ugonjwa wa akili.
Nurdin Ramathan ni miongoni mwa vijana aliye ona changamoto na kuigeuza fursa Kwa kujikita Katika ususi.