Dodoma FM
Dodoma FM
13 May 2026, 16:51

Mkutano huu ukalete tija kwa maafisa mazingira wote kwa kutoa Elimu na kuelimisha Jamii kwa ujumla juu ya maswala ya Taka.
Na Anwary Shaban.
Wananchi wametakiwa kutambua kuwa Taka ngumu ni mali, hivyo wanaweza kuzitumia na kuzirejeleza ili kuweka mji safi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi Ya Waziri Mkuu Tamisem Mhe.Pro.Riziki Shemdoe wakati akifungua Mkutano Wa Mwaka,wa Tathimini ya utekekezaji wa afua ya udhibiti wa taka Ngumu na usafi wa Miji jijini Dodoma.
Akizungumza wakati akifungua mkutano huo Pro.Shemdoe amesema Inakadiriwa kuwa uzalishaji wa taka duniani utafikia kiasi cha tani bilioni 3.04 Mwaka 2050 hii ni kutokana na ukuaji wa miji, mapinduzi ya kiviwanda na ongezeko la idadi ya watu. Aidha, zaidi ya aslimia 33 ya taka zinazozalishwa duniani hutupwa katika maeno yasiyo sahihi (open dumping)
Hali haiko tofauti sana hapa nchini, ambapo kuwekuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji wa taka kwa sababu zilezile za ongezeko la watu, ukuaji wa miji, ukuaji wa viwanda na biashara nchini. Mathalani hapa nchini kwa mwaka zaidi ya tani milioni 8.3 huzalishwa kila Mwaka ambapo 50.8% yataka hizo hazikusanywi, hivyo zinatupwa katika maeneo yasiyo rasmi. Hivyo iko haja kwa halmashauri nchini kuongeza uwezo wa kukusanya taka hizo ili kuweka miji safi, kulinda mazingira na afya ya jamii.

Amesema serikali imeendelea kuchukua hatua za kuimarisha mifumo ya udhibiti wa taka ngumu na uimarishaji usafi nchini kwa kuhakikisha kwamba Halmashauri nchini zinatenga fedha toka mapato ya ndani kwa ajili uendeshaji wa shughuli za usafi kuanzia asilimia 10 – 15.
Pia amesema baada ya miaka miwili mitatu nchi yetu tuwe tumefika kwenye Lengo la kuifadhi taka kutoka maeneo ambayo yanazalisha taka tukifanya hivyo tutakuwa tumeongeza thamani kuanzia pale maeneo yanayozalishwa.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Pro.Tumaini Nagu amesema udhibiti wa Utupaji taka unaweza kupungua kuanzia asilimia 30 hadi 40 ususani magonjwa kama Malaria na magonjwa yanayofanana na hayo nw udhibitiwa kwa kuhakikisha mazingira yapo safi na salama.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amesema Mkutano huu ukalete tija kwa maafisa mazingira wote kwa kutoa Elimu na kuelimisha Jamii kwa ujumla juu ya maswala ya Taka.